Ijumaa , 24th Sep , 2021

Legend wa Bongoflava Dully Sykes brotherman anasema atoa mwanamke endapo atakuwa tayari hata kama ndoa yake itadumu kwa wiki moja lakini ataoa hivyohivyo.

Picha ya msanii Dully Sykes

Dully Sykes amefunguka hilo kwenye show ya MamaMia ya East Africa Radio, baada ya kushindwa kuoa mwanamke hata mmoja kati ya wanawake 6 tofauti aliopata nao watoto.

"Nitaoa tu, naamini kwenye kuanza watoto kwanza, unaweza kuoa halafu nyumba isifabarikiwe watoto, nitaoa nikiwa tayari, hata kama ndoa yangu itadumu kwa wiki moja ila nitaoa"

"Mama watoto zangu wote tunalea pamoja na tunashirikiana siyo kwamba natoa mahitaji peke yangu" ameongeza Dully Sykes