Rosa Ree afunguka kuhusu kupokonywa gari na nyumba

Jumatano , 7th Aug , 2019

Rosa Ree "Goddess Of Rap" kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu suala la yeye kupokonywa gari na nyumba alizopewa nchini Afrika Kusini.

Msanii Rosa Ree

Rapa huyo alipewa gari na nyumba mwaka jana 2018, ikiwa ni sehemu ya mkataba wake ambayo ilikuwa inamsimamia katika kazi zake iitwayo Dimo Prouduction.

Akizungumza kupitia EATV & EA Radio Digital Rosa Ree amefunguka kuwa,

"Hakuna kitu kibaya kilichotokea ila kila kampuni ina sheria zake na mnapokuwa mna mkataba basi kuna kuwa na makubaliano, gari na nyumba zilikuwa ni mali ya kampuni zilibaki ofisini kwa sababu ni mali za ofisi, mimi niliendelea kuhangaika kivyangu namshukuru mungu hakuniacha kinyonge sasa hivi nimepata vya kwangu".

Mwezi wa sita mwaka 2018, Rosa Ree alitangaza kupata dili la usimamizi katika kazi zake za kimuziki ambao ulimuwezesha kumpa gari, nyumba, pesa zenye thamani ya Milioni 400 pamoja na kuishi nchini Afrika Kusini.