
Ruby na mpenzi wake aitwaye Kusah
Akiongea leo kwenye DADAZ ya East Africa Television amefunguka kuwa, yeye amewahi kushuhudia mtu akimpigia simu mpenzi wake na kumwambia ameingia sehemu ya starehe wakati huo yeye yupo na mpenzi wake.
''Mimi sina mashauzi wala kiburi lakini sina marafiki na niko tofauti na watu wengi hata wasanii wenzangu na haimanishi mimi ni special lakini inanifanya niepukane na watu wabaya kwangu'', ameeleza.
Kwa upande mwingine Ruby amesema kuwa anajipanga kuachia EP yake kabla ya mwaka huu kusisha. ''Nipo naandaa ngoma zangu kwaajili ya EP na nitaitoa, kwahiyo sijatoa ngoma hivi karibuni kwasababu hiyo, ila kazi zipo watu wasubiri''.
Zaidi tazama hapa.