Ijumaa , 10th Jul , 2015

Kundi la miondoka la afro-pop la Sauti Sol kutoka Kenya limetua jana usiku nchini Uganda kwa ajili ya kufanya onyesho lao la kwanza kabisa katika ardhi ya nchi hiyo Jijini Kampala.

Wasanii wa kundi la Sauti Sol la nchini Kenya

Wasanii hao wa kundi hilo walilazimika kuchelewa kufika kutokana na sababu za kiufundi zilizolikumba shirika la ndege walilokuwa wakitumia usafiri wake.

Wasanii wawili tu wa kundi hilo Polycarp Othieno na Bien Aime Baraza ndio waliotua kwanza hapo jana ambapo wengine waliobakia watafika Uganda leo usiku.

Kwa kuongezea tu ni kwamba wakali hao wanatarajia kufanya colabo ya pamoja na staa mkali wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Tanzania Vanessa Mdee katika wimbo mpya uliobatizwa jina ‘Kama Kama Kama’.