Jumatano , 9th Sep , 2015

Wasanii wa kike wanao 'rap' kutoka Kenya, Shani, Lesynem Junior na Corinne Kahi wanaofanya kazi kama kundi chini ya
The P 31 Project wametua hapa nchini kutangaza kazi yao inayokwenda kwa jina 'Its Time'.

Wasanii wa kike wanaorap kutoka Kenya, Shani, Lesynem Junior na Corinne Kahi

Wasanii hao wametumia nafasi hiyo kutoa hamasa hususan kwa vijana kuamka na kuanza kushughulikia mipango yao sasa na
wameeleza kukua kwa muziki wa injili nchini Kenya, sambamba na mapokezi makubwa ya muziki wa Hip Hop kwa upande wa Gospel, ukienda sambamba na uchaguzi na mapenzi wa kizazi kipya.