Jumatano , 28th Aug , 2019

Msanii wa kizazi kipya Omary Ally maarufu kama Marioo, amesema hana mahusiano na wala hajawahi kuwa na mahusiano na mwanamke yoyote yule katika maisha yake.

Marioo ameyabainisha hayo leo Agosti 28, 2019 wakati akizungumza katika Kikaangoni cha EATV wakati akijibu swali aliloulizwa kuhusu mwenendo wake wa mahusiano.

"Sina mpenzi na sijawahi kuwa na mahusiano na mtu yoyote, sipigi nyeto na sio bikra, Ila nina njia zangu ninazozijua mwenyewe" amesema Marioo.

Aidha Marioo amezungumzia kiwango chake cha elimu ambapo amesema kuwa,  hakufika Sekondari ameishia darasa la Saba lakini hadi sasa alipofikia,  anajiona anayo elimu ya kidato cha nne.

Tazama mahojiano kamili hapo chini.