Ijumaa , 27th Mei , 2016

Wasanii mbali mbali na wadau wa sanaa wamejitokeza jana katika siku ya kuzindua rasmi mchakato kuelekea siku ya msanii itakayofanyika Oktoba 29, kwenye ukumbi wa Alliance Francaise Upanga.

Wasanii wa Bongo

Akizungumza na eNewz mgeni rasmi ambae alimuwakilisha Waziri wa Habari Utamadunu na Michezo, Katibu wa wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel alisema kuwa sanaa ina nguvu kubwa katika jamii ndio maana wasanii wanatumika mara nyingi katika kampeni na matamgazo ya biashara.

Mahadhimisho hayo ya siku ya msanii ambayo yatafanyika katika ukumbi wa Alliance Francaise Upanga huku yakiongozwa na kauli mbiu isamayo "Sanaa ina nguvu".