Jumatatu , 12th Nov , 2018

Msanii Lady Jayde ambaye ni mkongwe kwenye game la bongo fleva na aliyejiwekea misingi imara, amekuwa tofauti na wasanii wengi wa kike bongo kwenye masuala ya mitandao ya kijamii, kwa kufollow watu watano tu kwenye acount yake.

Kwenye acunt yake ambayo imethibitishwa na instagram, Jaydee ana followers milioni 2.5, lakini yeye amekuwa akiwafollow watu watano tu, ambao watatu kati yao ni acount zake mwenyewe, mmoja akiwa ni msanii wa Uganda Juliana Kanyomozi, na moja ya msanii wa Tanzania Khadija Kopa.

Ukiangalia acount hizo ambazo anafollow ni pamoja na acount yake ya mapishi, (Ladyjaydee recipe), acount yake ya matamasha (Ladyjaydee Liveconcert), na acount yake ya show ya reality ambayo kwa sasa haiko hewani (Lady Jaydee diaries).

Kikubwa aMbacho mwandishi wa habari hii hakikutarajia ni kukuta msanii huyo ka unfollow aliyekuwa mpenzi wake msanii wa Nigeria, Spice Musik.

Kitendo cha Jaydee kumfolow Khadija Kopa ni kama heshima kubwa kwa Malkia huyo wa Mipasho, kwani ni mmoja ya wasanii ambao LadyJaydee alishawahi kusikika akisema anamkubali zaidi.