Whozu ajibu mapigo kwa Tunda, atoa kubwa kuliko

Jumamosi , 18th Jan , 2020

Baada ya kuwepo na taarifa za kuachana na mpenzi wake ambaye ni video vixen Tunda, msanii Whozu amesema hatamani kusikia chocote kuhusu Tunda, pia hampendi tena kilichobaki ni kumheshimu tu.

Kwenye picha ni Msanii Whozu, na video vixen Tunda

Whozu amesema hayo kupitia show ya "Friday Night Live" ya East Africa TV, kinachoruka siku ya Ijumaa kuanzia 9:00 kamili hadi 5:00 usiku, baada ya kuulizwa kinachoendelea kwa sasa kati yake na Tunda.

"Wao ndiyo wananiuliza kuhusu Tunda, mimi sitakagi kuongelea vitu hivyo, hata awepo na m-South Africa atajua mwenyewe, simpendi tena  namuheshimu tu, yeye yupo kwenye hizo kazi zake anazozifanya na huyo mtu wa Nigeria nafikiri watu wataelewa tu nini namaanisha, ila tupo poa tu hakuna kitu kinacholeta tofauti" ameeleza Whozu

Wiki iliyopita Tunda alimpost mwanaume mwingine kwenye mtandao wa Instagram aitwaye Otike ambaye ni raia wa Nigeria, kisha akaweka alama ya upendo na kuandika "povu ruksa".

Penzi la Whozu na Tunda limedumu kwa muda wa mwaka mmoja na miezi kadhaa, pia ndiyo mwanaume ambaye amekaa naye kwa muda mrefu kwenye historia ya watu aliokuwa nao kwenye mahusiano.