Mkuu wa mkoa atangaza msako 'guest house'

Ijumaa , 26th Apr , 2019

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ametangaza vita kwa wanawake wanaoingia Mkoani humo kwa ajili ya kufanya biashara za ukahaba.

Agrey Mwanri ametangaza vita hiyo baada ya kupata taarifa ya ongezeko la watu hao katika maeneo ya miji wakati wa usiku, na kusababisha migogoro kwenye baadhi ya familia.

Mkuu wa MKoa afunguka zaidi

 

“Nitasaka 'guest house' zote, na haya ni maagizo ninayatoa kwa wakuu wangu wa wilaya, wakurugenzi wangu wa halmashauri wa wilaya, hawa watu hawa watatuvurugia mambo sana wanakuja kuuza miili na tutakwenda hadi kwenye hizo geto na vita hivi tutavishinda kwa uhalali wa vita yenyewe”, amesema Agrey Mwanri.

Agrey Mwanri amesema kwamba kama mtu anayetaka kukaa mkoani humo akae kwa adabu, na sio kupageuza sehemu ya kujiuza.