Jumanne , 9th Jul , 2024

Toka Julai 3/2023 mpaka leo hii ni takribani mwaka sasa tangu kampuni ya ''Meta'' ilipotambulisha Application ya Threads ikiwa kama mpinzani wa application ya ''X'' ambayo zamani ilikuwa ikifahamika kama Twitter

 

Jambo la kushangaza zaidi, unaweza kuhisi mtandao huu umepoteza mvuto hata watumiaji lakini kwa uhalisia hali haiko hivyo; muda huu ambao unasoma andiko hili fahamu kuwa kwa mwezi Threads inajumla ya watumiaji hai Milioni 175.

Takwimu hizo ambazo zimetolewa na mmiliki wa mtandao huo Bilionea Mark Zuckerberg hazijataja namba husika kutoka kwenye maeneo tofauti, ila India imehesabika kuwa na idadi kubwa zaidi ya watumiaji hai wa mtandao huo.

Picha:  The New York Times