Jumanne , 16th Jul , 2019

Kumekuwepo na desturi ya baadhi ya wanaume kunyonya maziwa ya wake zao wanapokuwa wamejifungua, kitendo kinachoelezwa kuwa ni ukatili wa kijinsia wanachofanyiwa mama na mtoto.

Unyonyeshaji

Juma la kwanza la mwezi Agosti kila mwaka, huwa ni wiki ya siku ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama duniani, katika kuelekea wiki hiyo wanaume wameaswa kuachana na tabia hiyo kwakuwa inawanyima fursa watoto wadogo.

Hayo yameelezwa na Afisa Lishe wa Mkoa wa Iringa, Neema Mtekwa alipokuwa akizungumza katika warsha na waandishi wa habari, amesema wanaume wenye tabia za kunyonya maziwa ya wake zao wakati wakiwa wananyonyesha hawawatendei haki watoto kwani wao hutegemea maziwa ya mama pekee kwa kipindi chote cha miezi sita ya mwanzo.

Maziwa ya mama ni kwa ajili ya mtoto, ila kuna tabia ambayo inasemwa na bado haijafanyika utafiti wa kina, kwamba wapo baadhi ya wanaume wanapenda kunyonya maziwa ya wake zao wakijifungua, maziwa ambayo ni maalumu kwa ajili ya mtoto. Huu ni ukatili mkubwa dhidi ya mtoto”, amesema Neema.

Wiki ya unyonyeshaji duniani imewekwa kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto mchanga na mdogo.