Alhamisi , 5th Mei , 2022

Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelloti amekuwa kocha wa kwanza kufika fainali tano za michuano ya Ulaya (Uefa champions league) sambamba na kuweka rekodi ya kocha wa kwanza kufika fainali zaidi ya moja na klabu mbili tofauti kwenye michuano hiyo

(Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelloti)

Ancelloti mwenye umri wa miaka 62 maarufu kama “Don Carlo” aliiongoza klabu ya Ac Milan kwenye fainali tatu na kushinda mara mbili mnamo misimu ya (2003,2005 na 2007) huku kwa Madrid itakuwa ni mara ya pili baada ya kuifikisha fainali  msimu wa 2013/14.

"klabu hii ina historia kubwa ambayo inatusaidia kusonga mbele ,tulicheza na mpinzani mgumu aliyetupa ushindani mkubwa ,sikufikiria kama tutapoteza mchezo na wala sikuwa na muda wa kufikiria hilo na kwa sasa nina furaha sana ya kuelekea mjini Paris kupambana na mpinzani mkubwa na nafikiri utakuwa mchezo wa kuvutia sana siku ya fainali “anesena Carlo Ancelloti “Don Carlo”

Hii itakuwa ni fainali ya tatu kwa Real Madrid na Liverpool kukutana baada ya fainali mbili za mwaka 1981 na 2018 huku kila mmoja akishinda kwenye fainali moja pindi walipokutana kwenye fainali za ligi ya mabingwa barani Ulaya.