Ijumaa , 7th Mei , 2021

Mcheza kikapu nyota wa timu ya Los Angeles Lakers, Anthony Davis amesema anaendelea vizuri  licha ya kupata maumivu kwenye mchezo wa usiku wa kuamkia leo waliopoteza dhidi ya watani wao wa jadi, Los Angeles Clippers waliopoteza kwa alama 118 kwa 94.

Nyota wa Los Angeles Lakers, Anthony Davies.

 

Maumivu aliyoyapata Davis yaliibua mashaka makubwa kwa mashabiki wa Lakers kuelekea kwenye safari yao ya kutetea ubingwa huo kwani tokea wamkose nyota wake Lebron James kwa michezo kadhaa kikosi hicho cha jiji la Los Angeles kimeporomoka hadi nafasi ya sita.

NBA itaendela tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo kumi, vinara wa NBA kwa upande wa Magharibi, timu ya Philadelphia 76ers itacheza na New Orlean Pelicans, Milwaukee Bucks watakipiga na Houston Rockets ilhali Portland Trail Blazers watacheza na Los Angeles Lakers.

Vinara wa NBA kwa upande wa mashariki, timu ya Utah Jazz watacheza na Denver Nuggets.