
Afisa habari wa Azam FC Jaffery Iddy Maganga amesema, wanauangalia mchezo huo kama sehemu ya mchezo mgumu kwani timu ya Kagera haipo katika nafasi nzuri na imejipanga kwa ajili ya kujinasua katika hatari ya kushuka daraja msimu huu lakini kwa upande wa Azam FC pia wamejipanga kwa ajili ya kuweza kuondoka na pointi tatu.
Maganga amesema, katika safari ya hapo kesho wanatarajia kuondoka na wachezaji wote hata wale waliokuwa majeruhi akiwemo mlinzi wao Pascal Wawa ambaye aliumia nyama za paja na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.