Alhamisi , 14th Jan , 2021

Ikiwa ni siku chache baada ya kusimamishwa kufanya mazoezi na timu yake ya Houston Rockets, James Harden, ametangazwa rasmi leo tarehe 14 Januari 2021 kujiunga na Brooklyn Nets ya NBA nchini Marekani.

James Harden

Harden alisimamishwa kufanya mazoezi na Houston Rockets kabla ya kusajiliwa na Brooklyn Nets baada ya kutoa kauli yenye mkanganyiko juu ya nafasi ya timu yake kufanya vizuri ligi hiyo ya NBA ya nchini Marekani.

“Kiukweli hatupo hata karibu kiuwezo na bingwa mtetezi LA Lakers na hata timu nyingine kubwa kwenye NBA, hatuna ubora, hatupo vizuri, hatuna muunganiko na hatuna vipaji vikubwa", amesema Harden

“Nina upenda huu mji, nimefanya kila kitu niwezavyo, hali hii haiwezi kutatulika”, ameongeza.

Baada ya Harden kusema maneno hayo hapo jana, uongozi wa Houston Rockets, ulioonekana kutokufurahishwa na maneno hayo ulimsimamisha mchezaji huyo kufanya mazoezi, Houston Rockets, imefungwa michezo 6 na kushinda 3 kwenye michezo 9 iliyocjheza msimuu huu NBA.

Usajili wa James Harden, kwenda Brooklyn Nets unamfanya Harden kuungana na mshambuliaji nyota wa timu hiyo Kevin Durant, ambaye walikipiga wote wakiwa Oklahoma City Thunder na Mliniz nyota Kyrie Irving wenye viwango vizuri hivi sasa.