
Haruna Niyonzima na mkewe Cassandra Rayan.
Kupitia mtandao wa 'Inyarwanda' wa nchini Rwanda, imeripotiwa kuwa jana Aprili 28 kiungo huyo wa Yanga SC na timu ya taifa ya Rwanda ameoa mke wa pili, ndoa iliyofanyika nchini Tanzania.
Pia kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa nyota huyo (jina tunalo) amethibitisha kuwa ni kweli ndoa hiyo imefungwa, ambapo amesema, "ni kweli ameoa na ni jambo la kheri kwao, hivyo nawatakia ndoa njema".
Niyonzima ana watoto watatu ambao awali aliwapata na mke wake Naillah Uwineza ambaye ni raia wa Rwanda.
Haruna Niyonzima ni mmoja wa watu mashuhuri nchini Tanzania, akiwa amecheza vilabu kadhaa vya juu ikiwa ni pamoja na nchini Rwanda kama vile Rayon Sports, APR FC, Etincelles na AS Kigali, pamoja na Yanga SC na Simba SC kutoka Tanzania.