Jumatano , 28th Nov , 2018

Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, ameripotiwa kuwa hawazi tena kuwa kocha mkuu wa timu zaidi tu anaitaka nafasi ya kuwa Mkurugenzi wa ufundi au kuwa kwenye bodi ya timu.

Arsene Wenger

Hatua hiyo imekuja ikiwa tetesi mbalimbali zinaendelea kuwa Mfaransa huyo huenda akatua katika klabu ya Bayern Munich ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwenye ligi kuu ya Ujerumani msimu huu.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ambavyo vimetajwa kuwa ni vya karibu na kocha huyo aliyejiwekea heshima ndani ya Arsenal vinaeleza kuwa havutiwi na kazi ya ukocha jambo linalopelekea ageukie upande mwingine.

''Anapokea maombi mengi sana kila siku kutoka klabu na timu za taifa mbalimbali lakini kwasasa hawazi kuwa na jukumu la kuwa meneja anatamani kuwa Mkurugenzi wa ufundi na huenda siku zijazo itakuwa hivyo", kimeeleza chanzo hicho mbele ya Sky Sports.

Hata hivyo chanzo hicho kiligoma kuweka wazi kama moja ya ofa alizopokea ni kutoka Bayern Munich ambayo inashika nafasi ya tano kwenye Bundesliga ikiwa nyuma ya alama 9 kutoka kwa vinara Borussia Dortmund.