
Arsenal imeweka rekodi ya kuwa timu pekee iliyoshinda michezo yote 6 ya makundi ya Europa League msimu huu
Washika mitutu wa jiji la London klabu ya Arsenal, imeweka rekodi ya kuwa timu pekee kushinda michezo yote 6 ya makundi ya michuano hiyo msimu huu na kufanya waliowengi kuwapigia chepuo la vijana hao wa kocha Mikel Arteta, kufanya vizuri zaidi kwenye michezo inayofuata.
Vilabu vingine 23 vilivyofuzu ni AS Roma, Slavia Prague, Bayer Leverkusen, Benifica, Granada, PSV Eindhoven, Braga, Lille, AC Milan, Villareal, Antwerp, Dinamo Zagreb, Hoffenheim, Red Star Belgraade, Molde, Maccabi Tel Aviv, Wolfsberger, AC Young Boys, SSC Napoli na Real Sociedada, Krasnodar, Club Brugge, Dynamo Kiev, Manchester United, Redbull Salzburg, Shakhtar Donetsk, Olympiacos na Ajax vilabu hivyo nane vimefuzu hatua hiyo baada ya kumaliza nafasi ya 3 kwenye makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Droo ya nani kucheza na nani katika hatua ya 32 bora ya michuano hiyo inataraji kupangwa siku ya Jumatatu tarehe 14 muda mchache baada ya droo ya hatua ya mtoano ya 16 bora ya michuano ya mabingwa barani humo kupangwa mjini Nyon Uswizi.
Ikumbukwe kuwa timu kutoka kundi moja na hata timu kutoka taifa moja haviwezi kukutana kucheza kwenye hatua hii ya 32 ya michuano ya Uefa Europa League.