Jumatano , 6th Jul , 2022

Kampeni za uchaguzi wa klabu ya Yanga zimeingia siku ya tatu leo na kushuhudia mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais Suma Mwaitenda akizindua ilani yake ya miaka 8 na kuomba kura kwa wanachama wa klabu ya yanga kwenye makao makuu ya klabu hiyo Jangwani.

Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais Suma Mwaitenda

Mwaitenda ametaja vipaumbele vyake kuwa atahakikisha kuwa na utawala bora pamoja na kuboresha uwanja wa Kaunda sambamba na kuhakikisha timu za vijana pamoja na wanawake zinakuwa na mafanikio makubwa .

"Kwa kuwa nina utaalamu na ujenzi jengo letu linavyumba vizuri ambavyo nikiviboresha tunaweza kuweka kambi ya wachezaji wetu ili tuepushe gharama za kukodi hoteli kwa ajili ya kambi’’ amesema Mwaitenda

Aidha Mwaitenda amesema haumizwi na kitendo cha mgombea pekee wa nafasi ya Urais Eng Hersi Saidi kuongozana na kumnadi mpinzani wake kwenye nafasi ya makamu wa rais ingawaje binafsi yupo tayari kufanya kazi na mtu yoyote iwapo watachaguliwa na wanachama wa klabu ya Yanga.

Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu mnamo Julai 9, 2022 katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kupata viongozi watakaoongaza klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 4 ijayo.