
Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson(Kushoto) akipiga mpira mbele ya kiungo wa Ubelgiji, Thorgan Hazard(Kulia) katika mchezo wa jana.
Maumivu aliyopata Jordan Henderson yanafanya orodha ya wachezaji wanaotumainiwa kwenye klabu ya Liverpool kufika tisa na kuzidi kumpasua kichwa kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp wakati akijiandaa kuwavaa Leicester City kwenye mchezo wa EPL Unaotaraji kuchezwa Jumapili ya wiki hii.
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema “Ni kweli Jordan amepata maumivu ya mguu na akahisi hawezi kuendelea na mchezo lakini hana uhakika kama ni kuchanika kwa nyama za paja”. Lakini atafanyiwa vipimo zaidi baada ya timu kurejea Uingereza, Aliongezea Southgate.
Wachezaji nyota tisa wa Liverpool wanaosumbuliwa na majeraha ni walinzi wote wa chaguo la kwanza, Virjil Van Dijk, Joe Gomez, Andy Robertson na Trent Alexander Anorld.
Viungo Fabinho, Thiago Alcantara, Alexander Oxlade Chamberlin na mshambuliaji Mohammed Salah ambaye ameripotiwa kupata maambukizi ya Ugonjwa wa Korona.