Simba SC,Yanga SC kukutana robo fainali ASFA?

Jumanne , 11th Mei , 2021

Droo wazi ya upangwaji wa timu zitakazokutana katika hatua ya robo fainali ya 'Azam Sport Federation Cup' inafanyika leo Jumanne hii majira ya saa 5:00 asubuhi.

Wachezaji wa Simba na Yanga wakiwa kwenye moja ya dabi ya kariakoo

Timu zilizofuzu hatua hii ni Rhino Rangers (Tabora), Biashara United (Mara) Mwadui (Shinyanga) Azam (Dar-es-Salaam) Yanga (Dar-es-Salaam) Dodoma jiji FC (Dodoma) Simba ( Dar-es-Salaam ) na Namungo ya Lindi.

Swali kubwa kutoka kwa wadau, je Simba SC na Yanga SC wanaweza kukutana katika hatua hii?
Jibu ni ndiyo kwa kuwa droo hii ni ya wazi na haki,itakuwa mubashara katika TV ya Azam saa 5:00 kamili yawezekana wakakutana itategezea muokota kitufe

Msimu uliopita Simba na Yanga walikutana katika hatua ya robo fainali na Wanamsimbazi wakaibuka na ushindi wa magoli 4-1 katika mchezo uliyochezwa katika uwanja wa Hayati Benjamin Mkapa jiji la Dar es Salaam na hatimaye akacheza fainali na Namungo na kufanikiwa kutwaa ubingwa

Michuano hii ya ASFA ambayo vilabu vya ligi kuu vinaichukulia kama 'njia ya mkato' kwa kuwa jumla ya mechi 5 hadi kuwa bingwa, ambapo utawapa uwakilisha nchi katika kombe la shirikisho barani Africa 'CAF'.