Jumatano , 6th Sep , 2017

Kocha wa timu ya TMT, Evans Davies Mwaseba amefunguka na kudai ushindani uliyokuwepo baina yao na Mchenga BBall Stars ulipelekea kufahamu matokeo mapema ya kuwa Mchenga BBall Stars atachukua kikombe hicho, japo kwa upande wao walijitahidi kupambana.

Timu ya TMT.

Mwaseba amezungumza hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha Kipenga kinachorushwa na EA Radio na kusema wapinzani wao bahati ilikuwa upande wao ndiyo maana wameweza kushinda huku akiwapongeza kwa kuweka historia.

"Hizi timu mbili zilikuwa na upinzani mkubwa kipindi zikicheza mpaka inapelekea hujui nani atashinda, japokuwa tulipocheza 'game' ya kwanza tayari ikajionyesha kwamba Mchenga BBall Stars watachukua hili kombe moja kwa moja na hawatafika hata ile 'game 5' lakini sisi kama TMT tulijipanga vizuri, na tukasema lazima tushinde kwa njia yoyote ile lakini mwisho wa siku katika mpira wa kikapu hakuna sare ya kufunguna lazima ipatikane timu ishinde", amesema Evans.

Wachezaji wa timu ya TMT wakiwa pamoja na kocha wao Evans aliyevalia sharti jeupe

Msikilize hapa Chini Mwaseba akiendelea kufunguka.