
Tatum ameshinda tuzo ya MVP ya Larry Bird kanda ya Mashariki
Tatum amefunga alama 26, pasi za kufunga 6 na rebound 10. Kwenye mchezo wa 7 wa fainali ukanda wa mashariki dhidi ya Miami Heat ambao wameshinda kwa alama 100 kwa 96.
Kwenye mfululizo wa michezo 7 ya fainali Tatam mwenye umri wa miaka 24 amekuwa na wastani wa kufunga alama 24.8, rebound 8 na pasi za kufunga (assists) 5.5 kwa mchezo. Tuzu ni mpya na Tatumamekuwa mchezaji wa kwanza kushinda na inabeba jina la mchezaji wa zamani wa Boston Celtics Larry Bird