Jumamosi , 1st Oct , 2022

Timu ya Tanzania ya mpira wa miguu kwa Walemavu(Tembo Warriors ) imetoka suluhu kwenye mchezo wake wa  kwanza wa mashindano  ya Kombe la Dunia 2022 dhidi ya timu ya Hispania uliofanyika leo Oktoba 1, 2022.

Matokeo ya leo yanaifanya Tembo Warriors kushika nafasi ya 3 ikiwa na alama moja sawa na Hispania inayokamata nafasi ya pili huku Uzbekistan ikikamata  nafasi ya kwanza wakiwa  na alama 3 baada ya kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Poland wa magoli 3-1. 

Mchezo huo umehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Lt. Gen. Yacoub Mohamed pamoja  na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi kwenye uwanja wa TFF RIVA mjini Istanbul, Uturuki.

Tembo Warriors inataraji kushuka dimbani kesho majira ya 11:30 dhidi ya Poland inayokamata nafasi ya mwisho wa kundi E huku michuano hiyo ikitaraji kumalizika mnamo Oktoba 9-2022