
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Yanga, Donald Dombo Ngoma.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga Jerry Muro amesema kuna taarifa ambazo zimesambaa zikidai nyota huyo aliyefanikiwa kufunga magoli 17 kwenye msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara anawaniwa na vilabu vya Misri na Afrika Kusini na yeye yuko tayari kujiunga navyo.
Muro amesema, Yanga bado inamkataba wa mwaka mmoja na Ngoma baada ya kumalizika kwa msimu huu na bado hawajapokea ofa kutoka klabu yeyote inayomtaka na hivyo taarifa za Ngoma kuondoka sio za kweli.
Hadi sasa Ngoma aliyetokea FC Platinum ya Zimbabwe ameshacheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara, FA Cup, Kombe la Klabu Bingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika ambapo ameonyesha kiwango kizuri kwa klabu yake ya Yanga.