Alhamisi , 6th Oct , 2022

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedrick Kaze amesema kuwa makossa ambayo waliyafanya msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa mapema yamewapa hasira ya kupambana kuyafuta.

kikosi cha Yanga

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga ilifungashiwa virago hatua ya awali kwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Rivers United.

Kaze amesema kuwa wanatambua mashabiki wanahitaji matokeo hata wachezaji nao wanatambua kinachohitajika ni ushindi.

“Kuanzia benchi la ufundi, wachezaji, viongozi na mashabiki wanahitaji ushindi hilo lipo wazi, makosa ambayo tulifanya msimu uliopita yametupa hasira ya kupambana kuyafuta kwa kupata matokeo mazuri.

“Ukiangalia aina ya wachezaji waliopo kikosini wote ni wazuri na wana uzoefu pia kwenye mashindano ya kimataifa ni suala la kusubiri na kuona kile ambacho tunafanyia kazi mazoezini kinatupa matokeo chanya,” alisema Kaze.

Mchezo wao ujao kimataifa Yanga ni dhidi ya Al Hilal unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 8.