Jumamosi , 19th Jan , 2019

Ikiwa zimebaki saa chache tu kuelekea mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kati ya Stand United wanaowakaribisha Yanga, ambapo kocha wa vinara wa ligi Mwinyi Zahera amesema mbinu anayotumia kupanga kikosi.

Kocha Mwinyi Zahera (katikati).

Akiongea leo kwenye kikao cha kabla ya mechi 'Pre Match Meeting', Zahera amesema kila kocha katika eneo lake huwa anatoa maamuzi ya nani aanze na nani asianze kisha yeye hupokea maoni na kushauri tu.

''Kocha msaidizi na kocha wa walinda milango huwa nawaomba vikosi vyao wanavyotaka vianze kila mmoja ananiletea, kocha msaidizi ananipa kikosi kizima na kocha wa makipa ananipa jina la kipa anayetaka aanze kisha nashauri na tunatoka na kikosi cha kwanza'', amesema.

Kwa upande mwingine Zahera amesema kucheza leo kwa kinara wa mabao kwenye ligi mpaka sasa Heritier Makambo, inategemea na vikosi vya makocha wengine hivyo lolote linaweza kutokea lakini tayari nyota huyo ameanzia benchi.

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo dhidi ya Stand United mchezo utaanza saa 10:00 jioni.

Kindoki, Paul Godfrey, Gadiel, Andrew, Yondani, Shaibu, Ngassa, Fei toto, Amis Tambwe, Haruna Moshi, Ajibu.

Akiba: Ibrahim, Juma, Haji, Makapu, Kaseke, Buswita, Makambo.