
mfano wa picha ya wananchi wakifanya kilimo
Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau wa kilimo,Mkurugenzi mtendaji wa taasisi inayojihusisha na kilimo Peter isare anasema Kama wananchi wakiamua kuwekeza kwenye kilimo tatizo la ajira na umasikini litakuwa ni historia nchini na kuacha dhana ya kusema kilimo hakilipi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi-JATU Mhandisi Dkt Zaipuna Yona amesema anaumia kuona vijana hawachangamkii kujiajiri katika sekta ya kilimo,ambayo ni mtatuzi wa tatizo la ajira hapa nchini.
'' Huu ni wakati wa Watanzania kubadilika kifikra ,na kufanya uwekezaji katika sekta ya kilimo ambayo inazalisha ajira nyingi,na kwa kufanya hivyo umaskini utaondoka'' Amesema Mhandisi Dkt Zaipuna
Zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wamejiajiri katika sekta ya kilimo,ambapo kinachohitajika ni elimu ya kuwekeza katika sekta hii na utafutaji wa masoko kwa bidhaa zinazozalishwa na wakulima.