Jumamosi , 14th Nov , 2020

Kocha wa AC Milan ya Italia Stefano Piloli amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona, klabu hiyo imethibitisha leo Jumamosi.

Stefano Piloli amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona

AC Milan imetangaza kuwa Pioli amekutwa na Covi-19 kufutia vipimo vilivyofanywa leo asubuhi, lakini anaendelea vizuri na kwa sasa amejitenga yupo karantini nyumbani kwake.

Majibu ya wachezaji na wafanyakazi wengine wa timu hiyo yameonyesha kuwa wote wapo salama hawana maambukizi ingawa leo kikosi hicho hakikufanya mazoezi ambayo yalihairishwa baada ya taarifa za kocha Pioli .

Vinara hao wa ligi kuu nchini Italia Serie A watarejea mazoezini siku ya Jumatatu ambapo watakuwa wanajiandaa na mchezo wa ligi unao fata dhidi ya Napoli Novemba 22.

Wiki iliyopita AC Milan pia ilitangaza takribani wachezaji wao watano walikutwa na maambukizi ya Covid 19 akiwemo golikipa Gianluigi Donnarumma winga Jens Petter Hauge.

Siku za nyuma pia Zlatan Ibrahimovic alikutwa na virusi hivyo mara 2 kabla ya kupona wachezaji wengine ambao waliwahi kukutwa na Corona kwenye timu hiyo ni Daniel Maldini, Matteo Gabbia na Leo Duarte.