Alhamisi , 29th Apr , 2021

Mchezaji kinara kwa ubora kwenye mchezo wa Tenisi upande wa wanaume Novak Djokovic hatotetea Ubingwa wa michuano ya wazi ya Madrid baada ya kujiondoa katika michuano hiyo.

Novak Djokovic ambaye ndiye kinara wa ubora Duniani kwenye mchezo wa tenisi upande wa wanaume akiwa kwenye majukumu yake.

Raia huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 33, amewaomba radhi mashabiki kwa kushindwa kwake kushiriki michuano hiyo huku akiwaahidi kuwa kuwa atashiriki mwaka ujao.

Michuano hiyo ilishindwa kufanyika mwaka jana kufuatia changamoto ya janga la Corona.

Djokovic amejiondoa kwenye michuano hiyo ziliwa zimesalia wiki nne kabla ya kuanza kwa michuano ya wazi ya Ufaransa itakayozana kutimua vumbi Mei 30 mwaka huu.

Hajawa na mwanzo mzuri mwaka huu ambapo wiki iliyopita alipoteza dhidi ya Aslan Karatsev kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Serbia na mapema mwezi uliopota alifungwa na Muingereza Dan Evans kwenye michuano ya Monte Carlo Masters.