Jumatano , 1st Jun , 2022

Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake watatu akiwemo Silvester Wenceslaus Nyegu, John Odemba Aweyo, Nathan John Msuya wamefikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya hakimu Mkazi Moshi  wa tuhuma kesi ya uhujumu uchumi

Kesi hiyo ni kesi namba mbili ya mwaka 2022 ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi kwa kutumia mamlaka ya uongozi wa Ukuu wa Wilaya akisaidia na wenzake wanne ambapo mshtakiwa namba tano hajafikishwa mahakamani hapo na  mpaka Sasa haijajulikana alipo.