
Tembo hao wamevamia maeneo hayo na kuharibu mimea huku wakijeruhi wananchi katika vijiji vya Kwamatuku, Komsala, Mbagwi na Mzeri wilayani humo
Kufuatia tembo hao wananchi wa vijiji hivyowamelazimika kuyahama makazi yao
Tembo hao wanadaiwa kutokea hifadhi ya Mkoamazi iliyopo katika wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro na wamedaiwa kuvamia maeneo hayo mara kwa mara na kusababisha vifo na uharibufu wa mazao ya wananchi shambani