
Baadhi ya wananchi waliohudhuria msiba
Inadaiwa mwanaume huyo aliachana na aliyekuwa mke wake lakini bado alikuwa anampenda, na kwamba alitekeleza unyama huo baada ya mke wake huyo kwenda kumsalimia baba yake mkwe (Baba wa Jesto), na wakati anamcharanga mapanga Baba yake alishuhudia tukio hilo na ndipo alipoamua kuwaua wote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kisimo A John Misalaba, pamoja na Mtendaji wa Kijiji cha Nyashoshi Esther Peter, nao wakaeleza namna wanavyolifahamu tukio hilo na kuahidi kufanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kuweka ulinzi shirikishi wa namna ya kuwajengea uelewa wananchi wa kuishi vyema kwenye ndoa na mahusiano yao.