Jumatatu , 10th Oct , 2022

Waziri wa maendeleo ya Jamii wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema katika kipindi cha mwaka jana pekee watoto wa  kiume wapatao 1,114 wamelawitiwa ambapo ni sawa na wastani wa watoto 93 wa kiume wanafanyiwa ukatili huo kila mwezi

Waziri wa maendeleo ya Jamii wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima

Waziri Gwajima ametoa takwimu hizo Leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike na kueleza kwamba asilimia 60 ya vitendo hivyo vinatokea kwenye makazi ya  familia

Kuhusu watoto kuolewa wakiwa na umri mdogo chini ya miaka 18 waziri Gwajima amesema tayari serikali kupitia wizara za kisekta imeanza kufanya mapitio ya sheria ya ndoana kwa sasa  tayari maoni yameshaanza kuchukuliwa na timu bado inaendelea kukusanya maoni ya wananchi  kwa hatua zaidi ikiwemo kufikishwa bungeni 

Katika maadhimisho hayo ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike baadhi ya wasichana wametumia maadhimisho hayo  kuiomba serikali kuondoa kodi kwenye taulo za kike huku wakikipongeza kituo cha EATV kupitia kampeni yake ya namthamini kwani imekuwa msaada mkubwa kwa mtoto wa kike ambaye amekuwa akishindwa kwenda shule wakati wa hedhi kwa kukosa taulo hizo za kike