Ijumaa , 14th Oct , 2022

Wananchi wa Mivumoni Madale mpakani mwa mtaa wa Lusambi na Makamba mkoani Dar es Salaam, wameiomba serikali kusikia kilio chao cha zaidi ya miaka kumi sasa cha kukosa maji na hivyo kulazimika kuchimba mashimo ardhini Ili kutafuta maji ambayo si salama kiafya.

Baadhi ya wananchi wa Mivumoni

Wakizungumza na EATV hii leo Oktoba 14, 2022, wamesema changamoto ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo imekuwa kubwa na imekuwa ikimuathiri zaidi mwanamke kwa kuwa analazimika kutumia muda mwingi kwenda kutafuta maji jambo ambalo limesababisha ndoa nyingi kuvunjika.