Kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Ebola kilithibitishwa katika wilaya ya Mubende mwezi Septemba mwaka jana
Shirika la afya duniani WHO limethibitisha taarifa hiyo ya kumalizika kwa Ebola Uganda
Kwa mujibu wa WHO, taifa hutangazwa kumaliza Ebola iwapo hakujatokea kisa chochote katika kipindi cha siku 42 mtawalia
Aidha WHO imesema Uganda ilisajili visa 142 vya Ebola, vifo 55, wagonjwa 87 wakiripotiwa kupona.

