
Ardern alichaguliwa mwaka 2017 alipokuwa na umri wa miaka 37, na kuwa moja kati ya wanawake wenye umri mdogo ulimwenguni kuongoza serikali na kuhudumu kwenye wadhifa huo kwa miaka mitano na nusu.
Tangu mwaka 2020 serikali ya Ardern imekuwa ikitatizika na umaarufu wake pia umekuwa ukishuka kufuatia mfumuko wa bei na mdororo wa uchumi unaoinyemelea nchi yake na kuibuka kwa upinzani wa kihafidhina