Waziri Mbarawa amekagua ujenzi wa daraja hilo la JPM na kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 64
Amezitaka mamlaka husika kuendelea kuimarisha ulinzi ili watu wasio waaminifu wasiendelee kuhujumu vifaa hivyo vya ujenzi yakiwemo mafuta ya dizeli yanayosaidia kusafirisha mitambo
‘Nimesikia sikia taarifa kwenye mitandao kwamba watu wengine wanaiba baadhi ya vifaa hasa mafuta pengine mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wameniambia wamelidhibiti sana hilo jambo lakini kwenye SGR kipande cha kutoka Isaka kuja Mwanza kuna hiyo changamoto"
"Muelewe wakiendelea kuiba haya material wanaiba pesa ya Tanzania sababu mafuta ni pesa ya serikali kwahiyo naomba sana sisi wenye jukumu tuendelee kulinda miradi hii ili ihakikishe kwamba vifaa vinavyokuja hapa kwa ajili mradi vitumike na siyo vinginevyo"
Meneja wa wakala wa barabara TANROADS mkoa wa Mwanza Ambrose Paschal amesema mkandarasi anatekeleza mradi huo usiku na mchana ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati

