Hakuna ripoti za vifo wala majeruhi.Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimeelezea eneo la nyumba za muda zilizojaa kwa karibu kama makazi duni ya mwisho ya mji mkuu.
Iliwachukua zaidi ya wazima moto 900 na helikopta kadhaa saa tano kuzima moto huo.
Rais Yoon Suk-yeol alitoa wito wa juhudi zote za kupunguza uharibifu na kuhamasisha wazima moto na vifaa vyote vilivyopo, kulingana na msemaji wake. Bw Yoon kwa sasa yuko nchini Uswisi kwa mkutano wa kilele wa jukwaa la kiuchumi duniani mjini Davos.
Chanzo halisi cha moto huo bado hakijafahamika, lakini pia eneo hilo limekuwa likikabiliwa na majanga ya moto na mafuriko, huku nyumba nyingi zikijengwa kwa kutumia miti. Kwa mujibu wa gazeti la Korea Times, Kijiji cha Guryong kimekumbwa na ajali za moto zisiopungua 16 tangu mwaka 2009.

