
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah
Makamu wa Pili wa Rais ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kichama mkoani Tanga ambapo amewaomba viongozi wote wa CCM kuhakikisha kwenye maeneo yao wanasimama kwenye misimamo ya pamoja ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto.
Aidha amesema kuwa jamii inaweza kuishi bila udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kama kila mmoja atatimiza wajibu wake ili kuweza kuondokana na matukio hayo.
"Kwenye mikoa yetu hii bado kuna changamoto ya udhalilishaji wa wanawake na watoto, bado vijana wanaendelea kudhalilishwa bado kina mama wanaendelea kudhalilishwa, naomba nichukue nafasi hii kuwaomba viongozi wote wa CCM sote tuko hapa kwenye maeneo yetu tuhakikishe tunasimama kwenye muelekeo mmoja wa kupinga udhalilishaji," amesema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Sanjari na hayo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amekiasa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga kuhakikisha kinawashughulikia watendaji wote wazembe wanaotumika kukichafua chama hicho na kuwataka viongozi mbalimbali kuwaeleza wananchi maendeleo yanayofanywa na serikali yao.