Michael Kadege ashinda urais TBF
Michael Kadebe ameshinda kiti cha Urais wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) baada ya kupata kura 58 na kumshinda Phares Magesa aliyekuwa anatetea nafasi yake ambaye alipata kura 8, kwenye uchaguzi uliofanyika jana Disemba 30, 2021 Jijini Dodoma.