Aguero kurejea timu ya taifa Argentina
Nyota wa zamani wa timu ya Argentina Sergio Aguero amefanya mazungumzo na rais wa chama cha soka cha nchini humo AFA Claudio Tapia juu ya uwezekano wa yeye kuwemo kwenye benchi la ufundi la timu hiyo itakaposhiriki kwenye fainali za kombe la dunia mwezi november 2022 nchini Qatar.

