Takwimu za Chama Simba ni balaa, mechi 6 goli 5
Kiungo bora wa Ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita Clatous Chama amezidi kuonyesha ubora wake katika soka la Tanzania baada ya hapo jana kufunga mabao matatu Hat-trick kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup na kumfanya awe amehusika kwenye mabao 8 katika michezo 6.

