Aibu kijana kukaa bila kazi - Rais Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameoneshwa kushangazwa na tabia ya vijana wengi nchini kwamba wakimaliza shule hukaa ndani na vyeti vyao wakisubiri ajira kutoka serikalini, badala ya kutafuta fursa za kazi ambazo zingewaingizia kipato.

