Ukiona umeteleza jiuzulu- Mwisho
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho, amempongeza aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, kwa kitendo chake cha kiungwana cha kujiuzulu na kusema ndani ya uongozi ukiona umeteleza jiuzulu, kaa pembeni, jitafakari na urejee upya.

