Yanga yatoa tamko kuhusu usajili
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa, amethibitisha kwamba timu hiyo haitoongeza mchezaji mwingine kwa masaa yaliyobaki ya dirisha dogo la usajili, baada ya kupata saini ya Yohana Mkomola pamoja na beki Festo Kayembe kutoka Balende FC ya DRC.