
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kusema uchaguzi huuu mpya wa viongozi ndani ya CCM, umedhamiria kujenga CCM mpya itakayofanya kazi kwa ajili ya Watanzania.
“Tusingependa kama umma wa CCM kuona uchaguzi huu kwa namna yoyote unanajisiwa kwa vitendo na mienendo ambayo inakwenda kinyume na mageuzi makubwa ya chama chetu, hii ni kauli ya CCM mpya Tanzania mpya, lengo ni kukirejesha chama kwa wanachama kuwa chama cha wanachama na kinachoshughulika na shida za watu wetu”, alisema Hamprey Polepole.
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM aliendelea kwa kusema kuwa sasa hivi chama kimejipanga kupata aina ya viongozi ambao ni waadilifu, ili kuijenga CCM imara zaidi, kuweza kuendelea kushikilia dola ya nchi.
“Chama chetu kimejipanga kupata aina ya viongozi ambao ni waaminifu, waadilifu, wachapakazi, wanyeyekevu, wanaweka mbele maslahi ya taifa na chama chetu, ni viongozi wapole lakini wakali sana kwa mambo yasiyo faa, ni viongozi ambao wapo tayari kuwatumikia watanzania, hawa ndio aina ya viongozi ambao wanachama wa CCM wanatuletea ambao watapitia katika uchauzi tunaofanya mwaka huu”, alisema Bw. Polepole.
Mwaka huu chama cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa halmashauri kuu ya chama hicho, ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.