Monday , 29th Aug , 2016

Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema amepandishwa kizimbani katika mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo na kusomewa mashitaka mawili.

Godbless Lema

Mwendesha mashitaka katika kesi hiyo ametaja mashitaka hayo kuwa ni pamoja kutumia mitandao ya kijamii kuweka ujumbe wa uchochezi kwa kuhamasisha watu kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku.

Amesema shitaka la pili ni kumtumia ujumbe wenye lugha ya kuudhi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, kwa njia ya Simu.
Amesoma ujumbe huo mbele ya mahakama kuwa ulikuwa ukisomeka “Karibu Arusha, tutakufanya kama……….”

Lema amekana mashitaka yote, na ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambapo kwa shitaka la kwanza alitakiwa kupata mdhamini na shilingi 10, na shitaka la pili dhama ni shilingi milioni 15.

Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 13 mwaka huu.

Hakimu anayesikiliza kesi ni Desderi Kamugisha wakati wakili wa serikali akiwa ni Innocent Njau.