Tuesday , 26th Dec , 2017

Waziri wa Habari Sanaa  Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mwanahabari nguli Mayage S. Mayage kilichotokea asubuhi jana tarehe 25 Decemba, katika Hospitali ya  Mbweni Misheni Dar es salaam

Dkt.Mwakyembe amesema kuwa tasnia ya habari imempoteza mmoja wa wanahabari wenye uelewa mkubwa katika uchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii nchini.

Waziri Mwakyembe ametoa pole kwa familia,ndugu na jamaa na wanahabari wote nchini na kuwaombea mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Marehemu Mayage S. Mayage enzi za uhai wake alikuwa Mhariri wa siasa katika kampuni ya Raia Mwema Ltd na kaimu Mhariri kampuni ya habari corporation Ltd ,hadi anafikwa na mauti marehemu Mayage alikuwa anafanya kazi katika kampuni ya Tanzama Newspapers Ltd.